, , , , ,

Sinema ya Karate

KSh 383.00

Kadiri anaingiwa na wasiwasi kutokana na mabadiliko katika tabia ya rafiki yake. Anashangaa anapomwona rafiki yake akitoweka kama moshi baada ya masomo ya kila siku kuisha. Kitendo cha rafiki yake kinamtia ari ya kutaka kufahamu ni kitu gani kinachomtoa mwenzake mbio. Juhudi zake za kutaka kujua anakoenda rafiki yake wakati wa mazoezi ya karate yanaambulia patupu. Kwa sababu hiyo, anaapa kufanya juu chini ili apate kujua kinachoendelea na sababu za rafiki yake kubadilika.

Guaranteed Safe Checkout

Je, Kadiri atapata kujua kinachomfanya rafiki yake kubadilika? Je, atafanya nini ili kuweka wazi kinachoendelea? Je, ni nini kitatendeka atakapogundua kinachoendelea?
Sinema ya Karate ni kisa cha kiupelelezi. Kisa hiki kinaangazia masuala ya malezi, elimu, uhifadhi wa mazingira miongoni mwa masuala mengine katika jamii. Kisa hiki kimesheheni mbinu na mitindo mbalimbali ambayo itamfaidi mwanafunzi katika kujenga lugha na ubunifu wake.

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Sinema ya Karate”

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shopping Cart
Scroll to Top